Ruka kwenda kwenye makala
🌱 KilimoElimu • Uzalishaji • Soko
⌕
Mwanzo→Kilimo
Kilimo • Mwongozo wa vitendo

FAIDA ZA MBOLEA YA MBOJI

Matumizi ya mbolea ya mboji katika kilimo cha mazao yana faida zifuatazo; Utengenezaji wa mbolea ya mboji hauna gharama na ni rahisi hivyo wakulima wa ngazi zote wanaweza kuumudu. Mbolea ya mboji huboresha…

FAIDA ZA MBOLEA YA MBOJI
Kilimo / Kilimo Tanzania
MUHTASARI1 min

Makala hii imepangwa kwa hatua zinazosomeka na kutekelezeka shambani.

Matumizi ya mbolea ya mboji katika kilimo cha mazao yana faida zifuatazo;
  1. Utengenezaji wa mbolea ya mboji hauna gharama na ni rahisi hivyo wakulima wa ngazi zote wanaweza kuumudu.
  2. Mbolea ya mboji huboresha muundo wa udongo unaopelekea kuwa na mzunguko mzuri wa hewa na maji katika udongo.
  3. Mbolea ya mboji huongeza virutubisho vinavyohitajika na mmea katika udongo na hivyo kuongeza mazao.
  4. Mboji huongeza uwezo wa udongo kutunza maji na hivyo kupunguza kasi ya ukaukaji wa udongo hasa katika maeneo yenye hali ya joto na yasiyopata mvua za kutosha.
  5. Mbolea ya mboji huweza kutumika kama mbadala wa mbolea ya samadi wakati wakuandaa kitalu cha mboga.
  6. Mbolea ya mboji huboresha afya ya mmea na kufanya uwe na uwezo wa kustahimili magonjwa.
PITIA
Kahawa Inayoleta Utajiri