Ruka kwenda kwenye makala
🌱 KilimoElimu • Uzalishaji • Soko
⌕
Mwanzo→Ufugaji
Ufugaji • Mwongozo wa vitendo

AINA MBALIMBALI ZA SUNGURA (RABBIT BREEDS)

Kuna aina zaidi ya 45 za sungura duniani kote. Aina maarufu zinazojulikana Afrika ya Mashariki ni hizi zifuatazo: AINA MBALIMBALI ZA SUNGURA (RABBIT BREEDS) 1. NEW ZEALAND WHITE: Sungura hawa ni weupe na rangi…

AINA MBALIMBALI ZA SUNGURA (RABBIT BREEDS)
Ufugaji / Kilimo Tanzania
MUHTASARI2 min

Makala hii imepangwa kwa hatua zinazosomeka na kutekelezeka shambani.

Kuna aina zaidi ya 45 za sungura duniani kote. Aina maarufu zinazojulikana Afrika ya Mashariki ni hizi zifuatazo:

AINA MBALIMBALI ZA SUNGURA (RABBIT BREEDS)
AINA MBALIMBALI ZA SUNGURA (RABBIT BREEDS)

1. NEW ZEALAND WHITE: Sungura hawa ni weupe na rangi ya machoni ni hudhurungi (Pink) iliyokoza karibu na nyekundu kama wanavyoonekana katika picha hapo juu. Hubaleghe mapema (miezi sita), huzaa watoto saba au zaidi na wanaweza kuwanyonyesha vizuri. Nyama yao ni laini na ngozi zao ni nzuri kwa kutengenezea vitu vya mapambo. Wakubwa wanaweza kufikia kilo 2-4.

 

2. CALIFORNIA WHITE: Ni weupe wenye weusi katika ncha za masikio, midomo, pua na mkiani. Wanatoa nyama nyingi (kilo 3.5- 4.5). Vilevile wanabaleghe haraka (miezi 6), wanazaa watoto wengi (7-11) na ni wanyonyeshaji wazuri, ngozi zao vilevile zina thamani kubwa.

CALIFORNIA WHITE
CALIFORNIA WHITE

 

3. CHINCHILLA: Wana mchanganyiko wa manyoya meusi kwa meupe na kuonekana na rangi ya khaki (grey). Thamani ya ngozi yao (pelt) ni kubwa. Wanazaa watoto wachache na huchelewa kubakekhe (miezi 9). Wanafikia uzito wa kilo 5-7. Sungura hawa wanapatikana katika rangi mchanganyiko kama rangi ya udongo na zilizofifia kuelekea weusi

CHINCHILLA
CHINCHILLA

 

4. GERMAN GIANT: Sungura hawa ni weusi tititi na wana sifa zile za New Zealand White.

Aina (kabila) zingine zinazopatikana katika nchi za Afrika ya Mashariki ni Flemish Giant, Angora (huzalisha sufi-fur), Earlop, Dutch, Agout, Chaqured Giant na Frank Vender.

GERMAN GIANT
GERMAN GIANT
PITIA
KANUNI SAHAHI YA ULEAJI WA VIFARANGA VYA KUKU