Ruka kwenda kwenye makala
🌱 KilimoElimu • Uzalishaji • Soko
⌕
Mwanzo→Kilimo
Kilimo • Mwongozo wa vitendo

HIZI NDIZO MBINU ZA KUZUIA WADUDU, NDEGE NA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO

Wadudu Wadudu wanaoweza kushambulia mazao ni pamoja na katapila na jongoo .Katapila Hukata ncha ya mmea inayokua Kudhibiti Kagua shamba mara kwa mara ili kutambua kuwepo kwa wadudu hao na kuwaua. Jongoo…

HIZI NDIZO MBINU ZA KUZUIA WADUDU, NDEGE NA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO
Kilimo / Kilimo Tanzania
MUHTASARI1 min

Makala hii imepangwa kwa hatua zinazosomeka na kutekelezeka shambani.

Wadudu

Wadudu wanaoweza kushambulia mazao ni pamoja na katapila na jongoo

.Katapila

  • Hukata ncha ya mmea inayokua

Kudhibiti

  • Kagua shamba mara kwa mara ili kutambua kuwepo kwa wadudu hao na kuwaua.

Jongoo

Jongoo
  • Hukwangua shina na kuacha michubuko

Kudhibiti

  •  Kagua shamba mara kwa mara na kuwaua.

Kuku

  • Huharibu mmea kwa kuparura juu ya ardhi na kusababisha kujeruhi na kukata mizizi. Uharibifu huu husababisha mmea kuwa katika mazingira rahisi ya kushambuliwa na vimelea kama Fusarium batatis ambao huozesha mizizi ya mmea.

Kudhibiti

  • Zuia kuku wasiingie shambani.

Konokono

  • Husababisha uharibifu zaidi kipindi cha mvua. Wanapotambaa kwenye mmea huacha utando, hasa katika sehemu inayochipua na kusababisha mmea kudumaa.

Kudhibiti

  • Kagua shamba mara kwa mara na kuwaondoa.
  • Weka mchanganyiko wa mbolea ya samadi na majivu kuzunguka shina la mmea ili kuzuia wasiweze kupanda juu ya mimea.

ANGALIZO: Ni muhimu kupulizia / kunyunyizia dawa uharibifu ukiwa mkubwa sana. Tembelea maduka ya Kilimo kwa aJili ya Ushauri Zaidi na kununua Dawa.

PITIA
Mchuzi wa Mvinyo kwa Wingi: Usafi, Ufungashaji, Vibali na Soko la Bidhaa ya Kilimo