Ruka kwenda kwenye makala
🌱 KilimoElimu • Uzalishaji • Soko
⌕
Mwanzo→Kilimo
Kilimo • Mwongozo wa vitendo

KANUNI ZA KUANDAA KITALU CHA MBOGAMBOGA.

        Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m (ama urefu unaoona wewe kuwa unakufaaa ila tu upana ubaki kuwa 1mita) . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi chambegu. Kiasi cha mbegu…

KANUNI ZA KUANDAA KITALU CHA MBOGAMBOGA.
Kilimo / Kilimo Tanzania
MUHTASARI2 min

Makala hii imepangwa kwa hatua zinazosomeka na kutekelezeka shambani.

        Tengeneza tuta la kubwa wa 1m x 2m (ama urefu unaoona wewe kuwa unakufaaa ila tu upana ubaki kuwa 1mita) . Urefu na idadi ya matuta hutegemea kiasi cha
mbegu. Kiasi cha mbegu kwa hectare moja ni kilo 6 au 2 kg kwa eka.

·         Weka samadi iliyooza vizuri kiasi cha debe moja au mchanganyiko wa mbolea ya TSP na CAN (200gm) kwa uwiano wa 1:1 kwenye tuta changanya vizuri na udongo.

·         Sia mbegu kwenye mistari kwa nafasi ya 1 sm x 20 sm. Tawanya mbegu vizuri wakati wa kusia ili miche isisongamane.

·         Funika mbegu na weka matandazo ya nyasi kavu juu ya tuta na mwagiliwa maji. Udongo unatakiwa kuwa na unyevu kiasi mpaka mbegu ziote.

·         Nyasi ziondolewe mara tu mbegu zikiota .

·         Miche itunzwe vizuri na kitalu kiwe katika hali ya usafi.

·         Miche imwagiliwe maji mpaka ifikie umri wa kupandikiza shambani.

·         Sehemu ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji.

KUMBUKA:siku za ukaaji wa mbegu kitaruni inategemeana na aina ya mbegu ama zao.