Ruka kwenda kwenye makala
🌱 KilimoElimu • Uzalishaji • Soko
⌕
Mwanzo→Kilimo101
Kilimo101 • Mwongozo wa vitendo

UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU

UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU: Ugonjwa huu husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli. Bakteria hawa huingia mwilini kwa mnyama kwa njia ya chakula au mara tu mnyama anapozaliwa au kuku anapototolewa. – Bakteria…

UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU
Kilimo101 / Kilimo Tanzania
MUHTASARI2 min

Makala hii imepangwa kwa hatua zinazosomeka na kutekelezeka shambani.

UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU

UGONJWA WA COLIBACILLOSIS KWA KUKU: Ugonjwa huu husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli. Bakteria hawa huingia mwilini kwa mnyama kwa njia ya chakula au mara tu mnyama anapozaliwa au kuku anapototolewa.

– Bakteria hawa huanza mashambulizi mara tu mnyama anapopata matatizo (stress) kwa vile kinga ya mwili hupungua.

WANYAMA HUSIKA:

• Ugonjwa hujitokeza hasa kwa vifaranga( kuanzia wiki 2-4), ndama, watoto wa mbuzi, kondoo, farasi mara tu baada ya kuzaliwa (Neonatal diarrhoea).

• Wanyama wakubwa huwa kama wabebaji wa vijidudu (Carriers) na kinyesi chao mara nyingi ndiyo chanzo cha ugonjwa huu.

DALILI KWA VIFARANGA:

• Kutokuwa na raha (depression)

• Kuacha kula

• Kuharisha uharisho mweupe

• Rangi ya kilemba na mashavu kupauka

• Vifo

VIFARANGA VIKIFA HUONYESHA DALILI ZIFUATAZO:

• Ini na bandama huvimba na huwa na vidoadoa vya damu (haemorrhage)

• Ukungu wa usaha kwenye ini, na vifuko vya hewa (Air sacs) kwenye mapafu

• Uchafu wa majimaji nje ya viungo vya mwilini.

DALILI KWA NDAMA, WATOTO WA MBUZI, KONDOO N.K

– Ugonjwa mkali (Acute form)

• Kuharisha mfululizo

• Kupungua maji mwilini

• Kufa ndani ya masaa 12

– Ugonjwa wa makali ya (wastani) kati (Subacute form)

• Kuharisha kwa muda mrefu – Siku kadhaa

• Kupungukiwa maji mwilini

• Kukonda

• Kufa kama tiba haikupatikana haraka

• Mnyama akifa utumbo (ndani) huwa umejaa makamasi (mucoid enteritis)

TIBA

KUREKEBISHA HALI YA MWILINI

(i) Upunguaji wa maji, madini na vitamini hurekebishwa kwa kutumia dawa za kufunga kuharisha Kaovit R na vitamini
kama vile vitalyt, Vitastress na dawa zingine kama Sodium, Glucose

PITIA
BANDA BORA LA SUNGURA - Jifunze Maarifa ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi

(ii) Wape wanyama wagonjwa chakula kizuri chenye protini ya kutosha

DAWA ZA KUTIBU

  • Doxycol katika maji ya kunywa

KINGA

1. Colirid – Kinga katika chakula: Dawa hii huzuia colibacillosis kwa kuua wadudu ndani ya mwili wa kuku/mnyama

2. Farmacid premix – Dawa hii huchanganywa na chakula na huzuia collibacillosis kwa kuua na kuzuia vijidudu (E.coli) katika chakula kabla ya kuliwa na kuku au mnyama husika.

– Ndama, watoto wa mbuzi n.k- Wapate maziwa ya mwanzo ya mama (colostrum) mara baada ya kuzaliwa, kama mama amekufa mtoto apatiwe ‘artificial colostrum’

– Vifaranga wapewe antibacterials ndani ya wiki moja baada ya kutotolewa.

– Usafi wa mazingira, vyombo na wahudumu.

– Wanyama wakubwa wasichanganywe na wadogo (newborns)